NAKUPENDA MAMA BY MABROUK


VERSE-I
We ndio mungu wangu wa  dunia
mama najivunia,kwa kila ninachofanya mama nitakusujudia.
Siwezi kukukana we ndio wangu mama,
usiku na mchana jua nakupenda sana.
Sijui nifanye nini au  nikupe nini,
yaani chenye uthamani wa kunileta duniani.
Miezi tisa nimekaa tumboni  mwako mama,
hukutaka kunitupa kisa ulinipenda sana.
Mama ulivumilia kwenye shida na raha,
ukavuta subira mpaka ulipo nizaa.
Ukanileta vyema na ukanipeleka shule,
ukutaka baadae nije nisumbuliwe.
 Kidogo ulichopata ulikula na mimi,
kikubwa nacho ukipata unamshukuru zaidi manani.
 Mama kwangu  unathamani tena zaidi maishani,
yani  kama dereva we umeshika usukani. 

CHORUS
Oooonhooo yeeeeeehhh,
i love you mamaaaaa
Sifa zote mimi  nakupaaaa,
kwa malezi bora sanaaaa
Toka siku uliyonizaaaa,
mpaka leo ni  mkubwa nimekuaaaaa*2      
VERCE-II
 Asubuhi na mapema mama unadamka,
unapita kuhangaika kote kutafuta pesa.
 Mvua inakunyeshea mpaka jua linakuchwea,
kote unahangaika ridhiki kujitafutia.
 Mama we ni dira yangu katika maisha yangu,
hasa ni mwongozo wangu katika maisha yangu.
 Bila we mimi sina mafanikio tena,
bila we mambo yangu yatakwenda mrama.
 Bila we mi si lolote si chochote,
ndio maana muda mwingi napenda tuwe sote(mamaa).
 Nikikumbuka kipindi cha utotoni,
kipindi ambacho homa zilikuwa haziniishi mwilini.
 Mama ulihangaika kila kazi ulifanya,
ulipita kuhangaika ili upate kuniponya.
 
CHORUS
Oooonhooo yeeeeeehhh,
i love you mamaaaaa
Sifa zote mimi  nakupaaaa,
kwa malezi bora sanaaaa
Toka siku uliyonizaaaa,
mpaka leo ni  mkubwa nimekuaaaaa*2
VERSI-III
 Shukrani zangu nakupa  mama yangu,
we ndio  ulionileta katika huu ulimwengu.
Mama ulikila udongo eti kwasababu yangu,
ulitafuna mpaka mkaa na haukujari wake uchungu.
Mama ulichukia samaki  na aina zingine za  mboga,
na mama nilikuchosha kila sehemu ulinibeba.
Pole kwa  usumbufu mama  niliokupatia,
tangu ujauzito kunizaa na  kunilea.
 Wengi walitamani kuwepo mpaka  leo,
lakini mama zao waliwaua kama kitoweo.
Hakuna mtu nnayempenda duniani  kama mama yangu,
nitazidi kukutukuza mpaka mwisho wa maisha yangu.
Mama  yangu ni mzuri mpole na msikivu,
tena ni mchamungu mtafutaji na mtulivu.
Mama nakupenda sana siwezi kusema kiasi gani,
sijui niseme nini kwa jinsi ninavyo kuthamini.
       
CHORUS
Oooonhooo yeeeeeehhh,
i love you mamaaaaa
Sifa zote mimi  nakupaaaa,
kwa malezi bora sanaaaa
Toka siku uliyonizaaaa,
mpaka leo ni  mkubwa nimekuaaaaa*2
     
 OUTRO
Aaaanhaa nakupenda sana mama aina cha kukulipa ila shukrani  zangu  pokea
 Ila amini nitakutunza,nitakulinda kwa wema ulionitendea
 Mabruki hapaaaa!!!
 Ambassador wa nachingwea

No comments:

Post a Comment