K.K.K by Roma ft Nicolazo

Verse1:
Wameweka mpira kwapani tayari nishawanawa
Ka napiga halafu nafinya namficha shinji kagawa
Suka weka kushoto maninja wakachimbe dawa
Nina ngunga kama ukoo usipimie hizo sha**
Aluta kontinua
Viva ngoma viva
Bwanamdogo anajiita over
Mamdogo anajiita diva
Ni freemason fever
This ridiculos
Wauza Papa nguva dili nao pepndcula
We si una mengi (it's okey)
me ntakusaga
Show zangu baunsa anacheza
Mchecheto ulimpata jaguar
We nianzishe kwenye show nisepe na kijiji
Promoter utapigwa mawe na wanaojiita magwiji
Mzee kasema hakupi namba na hutaki jiunga vinega
Dogo utasugua benchi hutaki sugua gaga
Mc hufuati misingi unarukia kama panzi
Usifakamie ukadhani maziwa nyingine zanzi
Sio vita ni changamoto
Karibu kikwetu kwetu
Chagua fursa ukipenda Ikamate twenzetu
Wanatugawa kimakundi watumeze
Ona anakonda family lahi wallah
Leo jide anamjua songa
Middleman mkishndwana cv anaitia gundu
Atakula nini mwanangu
Lini nitajenga bunju
Mkinizima nisikike nitaenda cheza kabumbu
Na Roma atabaki juu ata ukiminya mapu** ooh

(Chorus)
Karibu kwenye kalamu
We baba uliyepinda mgongo
Kiwete mwenye magongo
Tupa magongo unifuate
Karibuni kwenye kalamu
Mama uliyelala juu ya kitanda
Unawaza kwenda kwa mganga
Imani yako itakuponya
Karibuni kwenye kalamu
Umejikwaa na umeanguka
nishike mkono inuka Jikung'ute kisha njoo
Karibuni kwenye kalamu ooh
Karibuni kwenye kalamu

Verse2
Njaa ya madee haifanani na njaa ya ommy wa tupogo
Na show akikataa Izzo B atakwenda Ney wa Mitego
Huyu anaikataa laki
Yule anaifuata kwa basi
Yule watamfanyia fitna ang'ae kama almasi
Pamoja utatoka wapi kati ya mchicha na mbuyu
Wadau wana chenga nyingi kama walichezea Tukuyu
Na kufumba macho siyo njia ya kuikwepa ngumi ya uso
Nilipotoka ni mbali enzi nadandia mafuso
Unaweza sali uzae chema ukazaa shoga na msagaji
Mpagani akabakwa ikatunga mimba akamzaa padri
Hili Mungu atukuzwe wote hawakuja kumzika sharo
Hamuoni Yesu alilia alipokufa lazaro
Na kabla Yesu hajarudi angerudi Nyerere mzee
Ashuhudie madhabau yakigeuzwa uwanja wa harambee
Hawakemee baba askofu wachungaji mashekhe
Wanaogeuza injili mtaji washindwe na walegee
Ukisema ukweli wanakuzika kama analog kwenda digital
Nashukuru nahema Mungu niepushe na tindikali
Nafunga na kusali litania ya bikira Maria
Piteni mbali nimetumwa na parokia
Tusipigane mapanga kubishana nani achinje
Wananidiss na bado unialika kwenye kilinge
Usiponipiga me nitapigwa hata na bajaj za mwenge
Nina msimamo kama ** kama ** tongwe yeah yeah

(Chorus)
 Karibuni kwenye kalamu
Dada uliyemaliza chuo
Umepass na huna kazi
Vibebe vyeti nifuate
Karibuni kwenye kalamu
Nyuma ya nondo ya gereza
Sauti yangu iwafariji
Ipo siku mtatoka kisha
Karibuni kwenye kalamu
Ona wazazi wamekufa
we ndio baba we ndio mama
Familia inakutazama
Karibuni kwenye kalamu yeah
Karibuni kwenye kalamu

(Bridge)
Ona me mzalendo mwenye mapendo
Nakemea wenye biashara ya magendo
Wanasema wamepinda kama mizengo
Wanasinzia kwenye mijengo
Ona me mzalendo mwenye mapendo
Nakemea wenye biashara ya magendo
Wanasema wamepinda kama mizengo
Wanasinzia kwenye mijengo

(Verse3)
Kambarage hakuwa chadema lakini alivaa kaki
Kuna wabunge uwa najiuliza wanavuta bangi ya wapi
Bongo movie ni bunge movie Tuitazame tamthilia
Viongozi wanashuka hadhi kwa kugeuka mabondia
Kukosa amani sio mpaka ugombane na nchi jirani
Polisi akimuua raia ni vita vya ndani kwa ndani
Rasilimali isiwe mali ya serikali
Mwekezaji epuka mgogoro wa ardhi
Mkulima na mfugaji aliyepata zero form four
Mnamsukuma aende veta
Mnaamini umeme wa magari ndio unahitaji mazezeta
Yashinde majaribu jela uliyefungwa kwa hira
Sali milango ifunguke design ya Paulo na sila
Anakula kwa mipira anahema kwa mashine
Nani alitunza bikira hadi siku anampata mume
Kama uliupasua mpira usiuze mechi karatu
Kuwa mvumilivu wa subira kama mama anayecheza upatu
Binti ametega mimba na wewe unajiona shababi
Kakuona ganda la ndizi
Na kwako beki hazikabi
Kuwadi anamfunda mwali
Sina amani na huyu kungwi
Hiyo pesa ya mchango wa harusi bora nisagie mirungi
Kadi hawapewei so usiogope hayo magari wanahongwa
Shosti ukaibeba sembe kizembe china utanyongwa
Maisha foleni umangaribi uache ukaipande tonda
Kiulaini wanaiua meli ipo siku utaiua nyonga
Siogopi mainstream na post ya kuvuka boda
Wanangu wa boda boda pigeni nyie ndio masoulder I told ya
maadui wapo kimbiji Na me nimeaga Tanga navuka boda ya Msumbiji
Tongwe****oooh


(Bridge)
Ona me mzalendo mwenye mapendo
Nakemea wenye biashara ya magendo
Wanasema wamepinda kama mizengo
Wanasinzia kwenye mijengo
Ona me mzalendo mwenye mapendo
Nakemea wenye biashara ya magendo
Wanasema wamepinda kama mizengo
Wanasinzia kwenye mijengo

.......Tongwe records baby

No comments:

Post a Comment