sitaki demu lyrics - Juma Nature a.k.a kiroboto


Juma Nature


title:Sitaki demu
Artist:Juma Nature
writer:Juma Nature

(Verse 1)
Nakuomba usije kwetu mamdogo utatia hasara
Uyo mdogo wangu mwenyewe toka atoke shule hajala
Aaah bwana eh usinifate bwana
We si ukalale uwape mbu faida bwana
Hivi aliyekwambia uzime taa humu ndani nani
Kila ukija nyumbani we unaondoka
Kila ukija nyumbani we unaondoka
Nimetokea upande wa pili nmeenda kwa kina bashir
Na usije kwetu hakuna kitenge wala kanga
 Shauri ukija wazazi wangu watakuona mwanga
Nakumbuka ile siku ambayo umenisemelea kwa dingi
Ukadai ya kwamba me uwa nachanganya mitungi
Na kwenye kula ganja kilasiku sijivungi
Ukaondoka na cheko nyuma ukaacha kivumbi
Aya sasa unaona mwenzio umeniachia zogo
Mjeruhi wa simba
Chui mjeruhi wa mbogo
Umesababisha hata majirani wananitupia kisogo
Tena usinibishie ntakupa kidochi chi chi
Tatzo limenisumbua me sitaki unung'unike
Wakati inapita wiki me jombi hasinshike
Na usinilete zile zako za kike kike
Na kuanzia muda huu me naudhu usinshike
Afadhal demu mwenyewe ungekuwa unafunga domo
Hapo ningejipa moyo unalijua somo
Tena angalia sana usinizuge na shikamoo aya nimeghairi nenda kwa huyo huyo J.mo

(chorus)
Walimwengu walikwisha niambia kuwa demu wangu mimi hafai(hafai)
Mimi nikawabishia nikaona wao ndio hawafai
Hivi sasa me najuta sitaki demu sihitaji demu

(Verse:2)
Ukimchekea nyani shambani atakusumbua
Utavuna mabua na usiombee wenzio kujua watakucheka
Kipi kimegusa we kisusa uliyesuswa
Mpaka ukawambia wenzio unanirusha ''unanirusha''
Ukome kunzushia tena
Mkongwe naitwa kibra mwenye money hachunwi
Ili mradi nshapima nmeonekana sina ngoma
Msichana gani mhuni kila siku unaongwa laki
Sitaki demu ebu uko
huyu demu mtoto wa mzee mwalubadu yule mzee mvuv anayeongoza kwa kuvua ngadu
We mtu gani muhuni wanakujua njia zote

(chorus)
Walimwengu walikwisha niambia kuwa demu wangu mimi hafai(hafai)
Mimi nikawabishia nikaona wao ndio hawafai
Hivi sasa me najuta sitaki demu sihitaji demu

No comments:

Post a Comment