baada ya Asha Baraka kulalamika bosi wa mashujaa afunguka

baada ya boss wa band ya AFRICAN STARS (Twanga Pepeta) Asha Baraka kulalamika kwamba amekua akipokea vitisho vya msg, kupigwa chupa za uhai huku akidai pia kwamba watu kutoka vingunguti asiowafahamu walimfata dukani kwake na kumzomea, Vitisho ambavyo alisema vinatokana na Boss wa Band ya Mashujaa Opajo Hosea kuhusika kutuma hao watu.

Sasa leo Max ambae ni kiongozi mkuu wa band ya Mashujaa amesema maneno haya “nazikanusha hizi taarifa, Asha Baraka nadhani yeye ni mcha Mungu, aseme Ukweli tu manake sababu kubwa iliyozaa haya yote ni wanamuziki tuliowachukua kutoka TWANGA PEPETA ambapo mtu ambae alitakiwa kusema anatishiwa ni sisi kwa sababu ndio tumemchukulia wanamuziki, yani hii inaonyesha mama huyu ana tapatapa”

Max amesema kwamba “anaipandisha tu Mashujaa kwa kuiongelea, nafikiri angekaa kimya manake alikua yuko juu na sasa hivi anaanza kushuka, ajipange yeye na timu yake waangalie ni wapi wamekosea na sio kuleta challenge za kitoto namna hii, na kwa kuongezea tu wanamuziki wote ambao tumewachukua Twanga wao ndio walihitaji kazi Mashujaa”

No comments:

Post a Comment