LILIAN INTERNET ATAJA MKWANJA ULIOMSHAWISHI AHAMIE MASHUJAA BAND!

Lilian Internet kwenye moja ya show alipokuwa na twanga pepeta


Stori iliyoshika nafasi ya kwanza ijumaa iliyopita kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM, ilihusu band ya Mashujaa kuzidi kuchukua wakali wa muziki wa dance kutoka band ya African stars Twanga pepeta, ambapo meneja max wa mashujaa ndio alitangaza hizo habari Exclusive kwamba Wakali wawili waliowachukua walikwenda kuomba kazi wenyewe.

jana millardayo.com ndio ilkuwa ya kwanza kuzungumza na Lilian, hajazungumza na chombo chochote cha habari baada ya kuchukuliwa na Mashujaa.

Internet amesema sio kweli kwamba yeye ndio alikwenda kuomba kazi bali wao wenyewe Mashujaa ndio walimfata mara mbili na baada ya kuridhika na walichoafikiana ndio akaamua kujiunga nao kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo mshahara aliokua analipwa Twanga unatofautiana na wa Mashujaa kwa shilingi laki moja tu.

Lilian ameamplfy “walinipigia simu ila wakawa wanawasiwasi kwa kusema nyinyi bwana hamchukuliki kwenye ile band, mi nikawaambia kama kuna hela nzuri mi nahama wala sina shida, kitu kingine kilichonivutia kujiunga na Mashujaa ni kwamba nilivyokua Twanga pepeta nilikua sifanyi kazi kwa bidii sana, nilikua naona kuna uzembe flani hivi ila kwa Mashujaa mambo yatakua poa”

kwa kumalizia, Lilian amesema mbali na mkataba band hiyo ya Mashujaa imempa shilingi milioni tano kama donge nono la kumshawishi pamoja na kumlipia kodi ya nyumba kwa mwaka ambayo ni shilingi milioni tatu.


habari na millardayo.com

No comments:

Post a Comment