STEREO NA NIKKI MBISHI SIO LUNDUNO TENA

Nikki Mbishi na StereoMarch 2 2012 imeingia kwenye kitabu cha kumbukumbu za 2012 baada ya marapa wawili Nikki Mbishi na Stereo kutangaza kujitoa kwenye kundi la LUNDUNO.

Aliyekua wa kwanza kujitoa ni Stereo ambae aliamplfy kwamba “najua hizi taarifa zitashtua watu lakini inabidi wazikubali manake nilijiunga na Lunduno Mwenyewe na hata kujitoa nimejitoa mwenyewe bila kulazimishwa, mambo yamekua mengi mimi nasoma sasa hivi mwaka wa pili chuo cha Ardhi kwa hiyo time inabana, kitu kingine ni kwamba sitaki nibanwe na kazi nikashindwa kutekeleza majukumu ya Lunduno alafu watu waseme naringa, vilevile nataka pia kufanya mambo yangu mwenyewe, sijagombana na mtu yoyote, Nikki na One ni watu ambao nafanya kazi nao M-LAB studios na tutaendelea kuwa kitu kimoja kwa sababu tunafanya kazi kwenye record label moja”

Nikki Mbishi amesema sababu za yeye kujitoa ni kukinzana wenyewe kwa wenyewe, yani imetokea hawaelewani mara kadhaa sasa ili kuendeleza heshima, ni bora kila mtu achukue zake ili heshima iendelee kuwepo.

ujumbe aliondika Nikki Mbishi kwenye page yake ya FB
source:milliardayo.com

No comments:

Post a Comment