Blue aongelea moja ya plan zake kwa mwaka 2012
Staa ambae alijiunga rasmi na familia ya Bongo fleva baada ya kuachia single ya Blue Blue, Mr Blue ambae anazaidi ya miaka mitano kwenye familia hiyo, ameamplfy jingine kwa mwaka huu.


Blue amesema “nimeamua kubaki kwenye staili yangu niliyoitumia kwenye single zangu za mapozi, narudi, roho zinawauma, japo kurap ndio stail iliyonitambulisha kwenye blue blue”


ameamplfy zaidi kwamba “mwaka 2012 nimeamua kuimba tu, nitafanya nyimbo za kuimba tu kuonyesha uwezo, na walioiga stail yangu ya kuimba na ikawapa mambo mengi wanajulikana wengi na ninawatizama tu, ila mwenyewe nimerudi”


Blue ambae wiki tatu kutoka sasa atakwenda kukamilisha dili lake la kupiga show Malaysia, amesema kwenye kurap atafanya kidogo sana lakini kuimba sana ndio kazi kubwa aliyoipanga kwa sababu ana nyimbo za kuimba karibu album nzima.

No comments:

Post a Comment