agano jipya by suma mnazareti ft Staminah

[Suma]
Mistari imejaa ubabu, hadi mababa wanaamkia
ubibi kaitaka haraka, watakimbizwa hadi atalia
kama kila awamu walikula, awamu ya nne wamekomba
madogo wameiteka dira, watu wazima game mtasanda
utanganyika una kivuli cha ujinga tabu na shida
kijana akivaa msuli, basi ujana ushampoteza
nauli imepanda kidogo, kigamboni watu wanalia
bush ashabanwa ule mchongo, soon wataanza kuogelea
maduka ya dawa za siri, wateja wakubwa madada
ukihonga honga kiakili, usije ukadhani ulipendwa
money iligeuka power, ghadaffi akaachia nchi
wageni wanatesa wazawa, kariakoo imekosa weusi
mi nahitaji namba kumi, sio moja ntakosa stand
viongozi wameanza na umimi, hili taifa wanaliweka bond
tamaa ikizidi uwezo, mwili lazima utumike
shida ukii'use kama kigezo, hiyo sketi lazima ishuke


tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
moro na kigoma majembe ndo tuko mjini
[umetusoma, hujatusoma sikiliza track kwa makini]
[sema yeah!] staminah na mnazaleti
haina kupoa kila mchongo unajiseti
[sema yeah, staminah na mnazaleti] ah ah, ah ah

[Staminah]
hii sio system ya madilu, haina shobo kwa mademu
kingunge mtafute mwiru, ngombare ashasanda game
mistari sukari guru hii lazima itakunogea
ila mashaka yatakudhuru, usijaribu ku'compare
mzungu akijichubua ujue moyoni ana uAfrika
dogo usikimbilie kukua, omba wakukubalie kifikra
vesti ya mcheza summo, betina lazima ikupwaye
kitambo kama gurumo, mabeste nicheki baadae
kila mwembamba ni model, sharo usiishi kiisidingo
na kifo ndo mwisho wa nyodo, jipange uache maringo
nimezaliwa jangwani, kivipi unitishie ukame
mkulima, rudi shambani hii ndo mundu ya machame
kabwela, mwenye kitambi bepari utamtesa nani
kokote mi kwangu kambi, anthony unipe ramani
sadaka ni sadaka ila zaka iende kweisaka
mamlaka yenye dhihaka, nasaka mpaka waraka ah


tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
moro na kigoma majembe ndo tuko mjini
[umetusoma, hujatusoma sikiliza track kwa makini]
[sema yeah!] staminah na mnazaleti
haina kupoa kila mchongo unajiseti
[sema yeah, staminah na mnazaleti] ah ah, ah ah

[Staminah & Suma]
Ndevu zingekuwa ndio kimo, Osama asingeujua ugaidi
na mvi sio utu uzima, jipange uache ugaidi
juisi haipashwi wala mstimu haumwagiliwi
bubu acha magumashi, chunga usimfokee kiziwi

wanataja walikotokea ili waongeze mashabiki
mi kwetu ndo mwisho wa reli, ukifwata level hizi hufiki
ustaa bongo unapeperuka, ka trouser bwanga ya loketo
so ukipata weka jenga, ili kesho wasikuite kapeto

ukikumbuka ulikotokea, maasai utachana chupi
na usiogope kupotea kama njia huikumbuki
darasa, bila dawati gonga nyundo ya kilimo
mchungaji, tumia torati shetani akija na mzimu

yeah
upendo penda unapopendwa, usipopendwa stress zinatosha
upendo wa mke umezidi ndugu, mama mkwe mpaka kasusa
cha maana ndo chenye maana, kwa wenye maana bila dhana
wachanaji sio wale wa jana, wanaochana leo wana laana


tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
moro na kigoma majembe ndo tuko mjini
[umetusoma, hujatusoma sikiliza track kwa makini]
[sema yeah!] staminah na mnazaleti
haina kupoa kila mchongo unajiseti
[sema yeah, staminah na mnazaleti] ah ah, ah ah


No comments:

Post a Comment