songa lyrics by songa

[Intro]
Yeaah… Duke Tachez.. yeeah

[verse1]
Yeah, kwa uzima nafungua kinywa nachomoa hii habari
Naisoma kwa kina vina vinatoboa ka’ bikari
Nimepima homa kwenye roho ya hii sayari
Wanasema n’na ngoma eti nakohoa mistari
Sihitaji support kupost stanza nia
Verse ni lugha mbili ka’ noti ya Tanzania
Vibaraka wana njaa, bosi anawaza mia
Ni mkosi balaa, kitaa tozi anatanga njia
Mbwiga hasifiki kwa ubingwa wa busara
Ukiona giza na jogoo haliwiki ujue mida ya kulala
MC vipi? Mbona huwakilishi shida ya fukara?
Au umeshapata tija umesahau tiba uchwara?
Mdomo… hauachi tathmini ya amani ya mswaki
Mtoa roho angepokea rushwa maskini gani angebaki?
Stuck kwenye move mi’ ni mkali kwenye flow
Na-scratch maujuzi m’ ni chaki we ni black wall
Mzungu anaiga kwenye shida ndugu Mungu,
Narusha machungu zaidi ya miba ya nungunungu
Nyoa dungu huu ni msiba mbwiga tubu
Nimeshika rungu nyumbu anasinywa ka’ sungusungu!

[chorus]
Niite SONGA!
Kanuni ya harakati,
Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
Niite SONGA!
Thamani ya muwajibikaji,
Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

[verse2]
Wazazi wanasema nimeshakua
Ina maana… vibaya na vyema nimeshajua
Jua linazama tazama inanyesha mvua
Nakesha kwa dua kumuombea anayekesha akivua
Alfajiri inafika na mwezi unazama
Jogoo la Mbishi lawika na wezi wanahama
Yamaanisha zienzi tenzi kwa ujenzi salama
Uweze chutama japo kuna washenzi wanabana
Wanasema mi’ ni mkali ila why sisikiki?
Bei ya sukari inafanya ninywe chai na pipi
Rafiki… mnafiki hanifai kwa dhiki
N’nachomshukuru Mungu tu uhai silipii
Cheza pazuri, ukiweza eneza kauli
Wajinga wanatoa macho ka’ wamepoteza nauli
Tenzi shule kwa hizi tungo nikumbuke
Hizi verse nagawa bure kwenye midundo ya Duke

[chorus]
Niite SONGA!
Kanuni ya harakati,
Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
Niite SONGA!
Thamani ya muwajibikaji,
Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

[verse3]
Baba ananiambia… Maneno hayavunji kuti
Sawa nachana ila mbona flow zangu hazifumi suti
Mi’ mweusi roho yangu haifugi chuki
Dada anasema usiposoma mdogo wangu utarudi bushi
Meza ukweli kwa pressure uteme uongo
Palla anasema Mhaya nd’o kauleta umeme bongo
Kama husajiliwi jitahidi uchenze ndondo
Mwema Mungu sio Said anayesema ubebe gongo
Sifuri ndio inaanza na moja ndio ya pili
Cha ajabu ya pili inaanza na kwanza inasubiri
Hoja ya kishamba haina haja ya kuijadili
Hii ni hoja ya kijanja pata stanza na akili
Hii mic ni shamba na mimi ndio mkulima
Navuna ninachopanda na ulimi ndio unalima
Hapa utaganda huu sio Umwinyi na Ujima
Mzazi mwambie mwana mjini si pa kupima…

[chorus]
Niite SONGA!
Kanuni ya harakati,
Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
Niite SONGA!
Thamani ya muwajibikaji,
Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

Niite SONGA!
Kanuni ya harakati,
Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
Niite SONGA!
Thamani ya muwajibikaji,
Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

No comments:

Post a Comment