hisia by Nikki Mbishi, Stereo, Suma Mnazaletiyeah
yeah
yes
unga waya kwenye spika
kisha weka fire kwenye reefer
ntafutie malaya sinorita
mguu mdogo ntakupwaya kama sneeker
nafuu mgogo kuliko wahaya wanavos'fika
twende sawa, mi ni dawa kwenye fever
home sio kipawa, popobawa wala sinza
kama kawa ukipagawa nakuuliza
wazawa nawapaisha mpaka ulaya kama Visa
weka umakini kando ukose Bundle za ku'surf
dili na mgambo ili akuvunje ka bango chafu
mi ni star wa billboard na msomi mwanafalsafa
na slaa kama wilbroad
hamuoni bado mna'suffer?
hii ni original, ndo maana ina'sound kama demo
enzi hizo game iko original, underground walikuwemo
pure facts than a pure
ukimtoa duke ma'producer wengi wa bongo premature cunts
mitaani sionekani kama jini
dada yako anatamani kuwa na bwana kama mimi
mashetani yanaghani kwa imani kama dini
zao zipo hewani pole zama za 90
na pimp big kwa hisia kama Ben cussons
i think big naingia ubia na main persons
kama rapper ni soccer me footballer
the hood baller, haina ku'beep nina full dollar
don ka tage, na jambazi na blaze peace tu
dili si huna chako, ume'mess unajaza ukristu
nasema ukweli ambao matozi wanauficha
ubabeli ndo umefanya nmfeli words in pictureakili zangu sio fyatu nkisema watu sio wema
kilema, wakati hawautaki na upendo sio upendo tena
nimeona mapema, hawapendi kuona unahema labda unachechema
hauwezi unatema, ukipush unadema
mipango hiyo inabuma kisa jirani unafichwa gizani kwako
hata ukipita mibani ukatize nyikani
ili wakufute kwenye ramani, pesa ikukimbie kifupi ufulie..ka zamani
muumba akuchukie, tena akunyime thawabu, dhambi zao ulipie
mambo yakupindie bila sababu, kote wasimulie, upigwe majungu kama taarabu
hakuna ustaarabu, bila kosa wakushikishe adabu...yo
na kesho unawaza haupati majibu
unaamua kukaza na bado magumu yanasibu
unachanganya ladha tofauti za pombe balaa
usipagawe brotha jikaze ndo ilivyo mitaa
yupi utamuamini wengi wafitini ma'snitch
wapige chini treni itarudi relini skufichi
haina kufichana, kujuta kushika tama, sio juzi na jana
watu waamini kitu kazama
kichwani una mawazo demu wako keshakutosa
fedha hauna yule anazo aki'beep anatuma vocha
kata pochi upate penzi hauna kula uchochoro
utafanyiwa ushenzi kila unaporudi mgogoro
pigana na hela kisela maneno sio pungufu
ukisemwa hulazwi
songa mbele kichwa mkuki
toka, nduki! uso watupie, chuki wachukie. tena usiwanunie
sana wajutie, wakahadithie


nnachokumbuka alimuamini kama mchungaji wa kanisa
yote yanayosemwa mitaani hakujua kama yanamgusa
akaona bora afeli shule, mwisho akafaulu mapenzi
mashauzi ndo vile, mwishoni yamekuwa majonzi
hakujua yesu wa mapenzi mitaani watu wangemuita
aliyemuamini kama mpenzi kawa yuda leo yamemkuta
drop love kwenye usasa, so long ka bi kidude
unampenda kisha unamuacha, asikutapeli kama dude
leo anataka second chance ka Salvador Cerrinza
alishachezea first chance ka movie cheki anakonda
rahisi sana kukubali kile ambacho yeye anajua
hata kama atakuja feli kwa vitendo sio kuongea
anakumbuka game tough yeye na mpenzi walizocheza
leo ana'drop kama clove, uchaguzi daily wanammeza
kila anayesoma likizo sio kweli kwamba ana supp
watoto wanawapita kiuwezo watu wazima mpaka wana'STOP!
AH, we utaona unapendwa kumbe ndo unachunwa
we unaona unapanda kumbe ndo unavunwa
ushambandika kama sticker ukimbandua ndo unasepa
usije ukatekeka akakumwaga ka ana tipa
ah, nilipendwa mpaka wapangaji nyumbani wakawa wananuna
leo love imegeuka mtaji kwenye mzani watu wanapima
sio siri haya mambo nimeshayaona kijana
demu fulani kamteka mwana mpaka mia anabana
washatumia sana pesa kisha wakaja achana
demu kahongwa mpaka chaser kumbe kuna boya anambana
sio kila anayebeba begi ukadhani shule anaelewa


hii ni siri yenye laana kama tupu ya mzazi
kwa roho mkunjufu sitoruhusu utundu wazi
sizungumzi na mwana, nazungumza na mzazi
huu uzungu wa kuuzana kama ruzuku ya jambazi
kumbuka, wema watoto wakwepe mkosi
baba ana nyumba ndogo kigezo kubwa haitoshi
anazuga anakupa support Yuda eskarioti!
pochi inashinda kwa mchumba bi mkubwa ale karoti
ona kijana amekosa malezi kisa mama hana uwezo
baba yupo kwa mpenzi lisa, ama baba hana uwezo
na mama haiwezi shida enzi zimepita kisa ana mpenzi wa kumridhisha
kumbuka, haya maisha safari, pole kwetu waliokufa wamemaliza tayari
wasifasifa sio sifa jijali, njoo pata maarifa hii taarifa ya habari
ona watoto wanaomba wanakosa na wana njaa kwasababu wazazi waliponzwa
na tamaa
hili janga la jamii sio janga la jamaa, binti mwenye kilanga
kalamba dume la mtaa, hii ni.. kwako wewe rafiki ya kujihami
kama huna nia njema huwezi kuwa jirani
sina imani nawe usiwe na imani nami
kama sote si wanyama mi ni simba we ni nyani
ila usilie mama, kaza moyo we shujaa
ingawa dhiki iko uraiani naimani imeshiba njaa
kuwe na imani ile amani ipate nafasi
mchunge mwana wa jirani asidanganywe na fataki

No comments:

Post a Comment