sihitaji marafiki lyrics by Fid Q ft Vyonne Mwale

CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
 udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

VERSE1
haijalishi ulikua na wangapi bali wangapi uko nao
..washkaji ambao... kosa lako lao wakati hauna mafao/wanaokufikiria wewe muda ambao/ wenzao walionao wanafikiria wengine ndo wanao/now
kupata washkaji ukiwa na pesa... ni rahisi/
kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi mie sikufichi sihitaji urafiki na usupastaa/ukihit ndo unang'aa.. upishwe useat kwenye bar,upewe beat na Jr../ kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground/sikuhizi mabinti wanaomiss ni walionidiss mie sio mdau/
wanakubali mie ni mkali wanataka kuijua Mmwanza
ninayoitangaza nikiwa safari kama habari za kwanza/
U-N-I-T na prof Ludi walionifunza kukaza...
kwetu mbali.. sijui lini nitarudi? (C) Lokua kanza/
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

VERSE 2;
na usupastaa huwa ni feki.. utakung'arisha ukiwa na Market/
utakupatia senti,utapita juu ya red carpet/
utageuka young & restless, utakupa wanawake/utakupa mafake brethrenz.. kisha utaenda zake/kwahiyo power its not permanent.. huwa ipo kwa muda tu/respect ur own conglomorete... fikiri kikubwa tu/masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru/
wanazusha najiskia.. so im my own best friend/
sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man/
naweza nikakata ringi kiasi cha kutopay attention, lakini sio tajiri wakuafford kuua true friendship/
tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga/na hizi falsafa double double ajabu sio kinywa cha mjomba/
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

VERSE 3
rafiki wa kweli yukoje.. ni mkimya au anayechonga/yule aliyekupa jina?au pengine anayekuponda? anayezuia usidondoke au anayesubiria kukuokota?/au ni yule ambaye ukimuudhi anakutusi kabla hajaondoka?/ hakuna adui mbaya ka rafiki yako mwenyewe ambaye hajui.. ka yupo nawe.. au yupo kinyume na wewe/bora adui.. kama hachachawi utaenda muomba akuelewe/
ka buibui.. naweka tandu mtaenda kando mzingue?/
kwani machizi wenyewe wako wapi ambao wanastahiki niwape vyeo/ inabidi tu uwaache wakuwatch kwenye kideo/unakula nao happy leo.. kesho wanamtaka mkeo/urafiki sitaki.. hauletagi maendeleo../
nilitamani kuwa mjamaa niwe genge kama nature/
wachache niliowafanya wakang'aa wanayaweka maisha yangu in danger/
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

No comments:

Post a Comment