karibu dar by kala jeremiah ft Ben pol

(Verse1)
picha linaanza ka muvi ya solomoni
ghafla vumbi linazidi wajanja wanavaa miwani
hii ndiyo dar, karibu ila usijisikie nyumbani
hapo ubungo usinunue simu utauziwa sabuni
panda daladala tukutane buguruni
kuna watu wanapiga utadhania majini
mtaani usiku utaona rangi zote za bikini
wanauza miili ili wanunue wali maini
usicheke bro kwa sababu mimi si mr. bean
chunga wallet yako hapa kuna wizi wa mfukoni
haukawii kushuka kwenye gari hauna phone
kuwa makini uvukapo huku gari hazipigi honi
daladala zina bajaji inakesha macho
ka huamini ngoja usiku ndo uamini we thomaso
wasio na kazi wanashindia stori za freemason
wajanja wamepanga sinza, kino na tabata
mchana anazibua vyoo usiku anakula bata
usikojoe ovyo bro mgambo watakukamata
hii ndo dar, mbona unadata kabla hata hujapata
starter?

CHORUS (ben pol)
bata ni daily (daily)
karibu bushmen kaa chini tukupashe habari
shangaa mataa dar ugongwe na gari
dar es salaam ya sasaX2

(Verse2)
karibu sana kwenye hili jiji la joto
uswahilini chumba kimoja baba mama na watoto
si ulisikiaga mabomu ya gongolamboto
yalifanya rafiki yangu Adamu akafia ghetto
yaliacha kovu kubwa kama la mbagala
dar es salaama watu wengi tu hawanaga pa kulala
kama unataka mirungi twenzetu mitaa ya ilala
magomeni, na ujanja wangu wote niliitwa ----
watu wanaingiza pesa wakiwa ghetto wamelala.....
watu wengi toka waje hawajawahi kurudi kwao
sababu hawana nauli japo wamemiss ndugu zao
kuhusu kushinda na njaa hapa ndo zao
wauza sura wanaishi kwa kuuza madem zao
mama anauza bangi, baba amekata ringi anashinda
anacheza bao
wake zao wanazini kurisha watoto wao
vijana wao wanatembeza karanga, wanatembeza
maji, wanatembeza vocha siyo kwa mitaji yao
jioni wanakabidhi hesabu kwa bosi wao
hii ndo dar, ukipenda unaweza kuita bongo
machizi wakikosa hela ya bia wanakula gongo
siri haiwi siri uswahilini ukipata mchongo
wapangaji watakuandama bro mpaka utahama
(bongo)
ni majungu mixer wanga
utaenda tu kwa mganga utakapolala ghetto kwako
halafu ukamwagiwa mchanga

CHORUS (ben pol)
bata ni daily (daily)
karibu bushmen kaa chini tukupashe habari
shangaa mataa dar ugongwe na gari
dar es salaam ya sasaX2

(Verse3)
dar es salaam ingekuwa nchi rais angekuwa lowasa
huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa
usione watu wamependeza wengine hawana hata
mia
hapa mboga ni maharage, nyanyachungu na bamia
brazamen anatembea toka keko kwa mguu
anakwenda mlimani city kununua mkate tuu
(are you on facebook?) ndiyo maswali ya maduu
ukitaka demu wa peke yako kata mgomba lala juu
ukimuita dem wako baa, wanakuja 'crew'
utachunwa mpaka raba utabaki miguu juu
hapa bomba halijatoa maji mwezi mzima
hii ni uswahilini tu, wala si kwa jiji zima
twende mbezi au masaki yanatoka mwaka mzima
katiza kwa mtogole uporwe simu mchana
siku hizi mwanaume anavaa suruali ya kubana
siku hizi dada'ako ana kalio za kichina
ukimtafuta humpati ashabadili rangi na jina

CHORUS (ben pol)
bata ni daily (daily)
karibu bushmen kaa chini tukupashe habari
shangaa mataa dar ugongwe na gari
dar es salaam ya sasaX2

No comments:

Post a Comment