Fitna by wanaume halisi

(intro)
Halisi chimvu kundenge
Vancheche vya kuntazami
Kwa ajili ya kunipa hasiraa

(Verse1)
Umemponza mdomo sa kilanga komo
Kwani mambo aliyoyafanya bar kila mtu alishangaa
Kisa kwenye pombe alijiita ye shujaa
Me bwana mzaramo me naweza kumwangusha
Maana nikinywa ngano siku hizi zinaniyeyusha
Kumbe katoka ubanda
Njia nzima nzi wamemtanda
Yaani yanamtoka maganda
Chenchelenche
Ndio ulikuwa msemo wake
Kufanya vibweka vimbwanga ndio ikawa zake
Akaanza matusi na baadhi ya makuzi
Yaani juzi juzi tu kamtukana afande
Kuuliza eti kisa pombe
Kama hizo pombe unakunywa peke yako
Tofauti na wenzako
Tena kimpango wako
(Laughing)
Aua unacheeka ntakuchukua me

(Chorus)
Mdomo umemponza
Kashindwa kuelezea yaliyomkuta kule bar
Rafiki wamemtenga kwasababu ya matusi na fitina
Mdomo umemponza
Kashindwa kuelezea yaliyomkuta kule bar
Rafiki wamemtenga kwasababu ya matusi na fitina
Na fitna (fitna)
na fitna (fitna)
na fitna (fitna)
Na fitna (fitna)

(Verse2)
Chunga domo lako kuwa kama umekutana na simba mla nyama za watu
Usijifanye fyatu
wakati ukimkanyaga mende tu unatoka nduki unaruka
Eti nyoka uyoo (yuko wapi)
Unakimbia nini (nini)
Fitna umbea majungu
kukaa
Na kina mama
Unawaambia nini (umbea)
Hiyo fani siyo yako
Fani ya watu wa taarabu
Au dume siyo riziki
Halafu watu sijui wanakuaga nimapimbi (pimbi)
Eti msanii kaingia studio na ndala (ndala)
Na amevaa pensi
Akujua anayosema
kwenye facebook na twitter
Sijui kisa hela
alizopewa
na mameneja feki
Wasiopenda wa uswazi
mzomeeni uyo (oooooooh)
Sasa kazi kwake na raia wake
Anashindwa kulala shauri ya ujinga wake
Kazi kwake me sipo uko
Mchanga wa pwani huooo
cheza nao kidaruso
Panda panda

(Chorus)
Mdomo umemponza
Kashindwa kuelezea yaliyomkuta kule bar
Rafiki wamemtenga kwasababu ya matusi na fitina
Mdomo umemponza
Kashindwa kuelezea yaliyomkuta kule bar
Rafiki wamemtenga kwasababu ya matusi na fitina
Na fitna (fitna)
na fitna (fitna)
na fitna (fitna)
Na fitna (fitna)

(Verse3)
Ndugu wamemtenga na marafiki wamempotezea
Kisa akishakolea tu matusi anawatolea
Limemponza domo Mayai wamemgongea
Alijiona ye ndio bingwa
Akisha gonga miwa tu anajifanya amepinda
Kubaka kukamata kunga'ang'ania mapenzi
Ubabe babe kinguvu nguvu bin makame
Hizo ndio zilikuwa zake
Umbea majungu fitina kwake wenzake
Sasa kilanga komo
Umemponza mdomo
Kulonga kuna gundu (bwana we
Chonga sana
Kugonga sana kuloga sana
Imemcost gharama watu wamemkomba
Wamekwara Hata ndala mguuni hana
Yaliyomkuta bara anashindwa hata kuelezea
Kudadadeki

(Chorus)
Mdomo umemponza
Kashindwa kuelezea yaliyomkuta kule bar
Rafiki wamemtenga kwasababu ya matusi na fitina
Mdomo umemponza
Kashindwa kuelezea yaliyomkuta kule bar
Rafiki wamemtenga kwasababu ya matusi na fitina
Na fitna (fitna)
na fitna (fitna)
na fitna (fitna)
Na fitna (fitna)

No comments:

Post a Comment