mdudu by solo thang ft mr.blue

mdudu by Solo thang

INTRO
(DE FATALITY MUSIC)
YOU KNOW WHAT TIME IT IS
ITS YA BOY BACK (HELLO HELLO HALOOOO)
SOLO THANG (ULAMAA)
AAAAAH THIS TIME AROUND
I THINK WE NEED "DUDU KILLER" (LETS GO NOW)

(VERSE 1)
EYO NAKUPA MFANO NJAA ,NA HUYU MDUDU WANAFANANA
SI UNAKULA KILA SIKU ,ILA NJAA INARUDI TENA
MDUDU ANACHEZA NA FEELINGS DAWA KAIIMBA MARVIN GAYE
(SEXUAL HEALING?) , HAUPONI MDUDU YUPO EVERY DAY
SIO KUNGUNI ILA ,NAE ANAPENDA KITANDA
NDIO LOCATION KAMA MOVIE, ACTION- KUNG FU PANDA
YE ANAPENDA NJIA PANDA KAMA UMBO LA MANATI
NDANI YA FIKRA KAKUJAZA KUWA, NISHATI MIHADHARATI
SIO FUNDI BILA SPANA NA, ANALEGEZA MACHO
HAKITOSHI ULICHONACHO SHARTI UPATE CHA MWENZAKO
YE NDIO CHANZO CHA MAYAI ALIPOMVA KUKU
NDIO KISA JOGOO HUWIKA WEWEEE MAMBO IPO HUKU
HAICHEKESHI WE UNACHEKA, NDIO UJUE TAYARI
HAKUNYESHI WE UMELOA USIJISHIKE TAFADHALI
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI??

(CHORUS)
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!

(VERSE 2)
SI BORA ANGEKUA PANYA UWEKE SUMU AMA MTEGO
PALE PALE KWENYE SHIMO HAHAAAA NDAGA FIJO
WATU NATEMBEA NA "PUMP" KAMA MAFUNDI BAISKELI
KAZI KUJAZA WATU UPEPO NA "BLADDER' ZINAJAA KWELI
HANA SINDANO SIO DONDORA USEME MPIRA KAUTOBOA
BILA ZANA USICHEZE RAFU, REFA KADI ASIPOTOA?
WE HAMIRA YE NI NGANO LAZIMA MMOJA ANAVIMBA
OGOPA SANA HUYU MDUDU ANATISHA KAMA SIMBA
KANGA MOJA NDEMBE NDEMBE ETI LAKI SI PESA
NA HAUWEZI KUISHI KAMA BURUDA BROTHER KAKA UTAJITESA
ILA MDUDU AKIKUPA NGOMA NENDA KANUNUE GUITAR
NDIO SAFARI UNAENDA ANZISHA BENDI KAKA FUTI SITA
SIO MBU USEME UTAPATA MALARIA
YE ANASAMBAZA UGONJWA AMBAO UNAITWA SEX-ERIA
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI??

(CHORUS)
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!

(VERSE 3)
UKIBANWA NA KIKOHOZI, NI LAZIMA UKOHOE
VIPI UKIBANWA NA MDUDU JIBU NENDA KAKOKOTOE
JAMAA KASHIKIWA PANGA AKAAMBIWA LAMBA MCHANGA
AKAGOMA AKATOKA NDUKI BREKI YA KWANZA KWAO UPANGA
JOLY, KAMKUTA DEMU, YULE DEMU AKAONYESHA SHANGA
HADHARA NDIO IKAWA CHUMBA!, MAANA MDUDU KASHAPANDA
SIO KWAMBA ALIKUA NA NJAA, ILA 'SHAWTY" KALA KONI
SI ANA KIU? MPE MAJI SASA BROTHER KULIKONI??
YEAH SIJAPATA KUONA MKATE MGUMU MBELE YA SUPU
VIPI NGOZI ZA UDONGO MZIGANDISHE KAMA SUMAKU?
INGAWA UMBO SIO CHAKULA, WATU UDENDA UNAWATOKA
UTASKIA KASHATAFUNWA, JIULIZE MWILI BANZOKA?
HUU MCHEZO USIO NA DRAW, LAZIMA MTU APIGWE BAO
UCHU KAMA MPENDA NYAMA, HAWA WADUDU NDIO ZAO
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI?

(CHORUS)
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!

No comments:

Post a Comment