siri ya mchezo by Fid Q ft Juma Nature

(verse1):Fid Q
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo
sikuwa na  umuhimu kihivyo
stimu  zikanipa elimu ya Biko
Kimaandiko
kimistari..
hadi fans wanascream nikirap
sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop
Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua
pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa  #teamMabiiitoz
Achana na  power window.. sijui  rimz za dimpo 
haileti bingo, mshiko?  Star ishi simple
sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui  kama
wadau hupendelea kukuona hivyo
bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu
jikombe ugongwe…mtaaa  ukuone hauna ishu
ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa
mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi
je hizi track za  harakati ni ujinga
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji
na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..
sio kipaji  kama  Kubanda eti unachana kigumu
kisa  track ikivuma sana kwenye chati  haidumu
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA.
baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA
NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJAN 
najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani
labda kubisha na wakinitisha najihami
inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani
 ‘’ Pole MAPROSOO’’ uhujumu –uchumi umefanya umetubu
WAZEE ni  wahuni  hadi soo waay back before SUGU
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu
na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu
kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu
huo ni utumwa pia
Unafanya  vijana  wanaumia.
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia


CHORUS:  ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata
komaa… kaza.. kisha utapata
Siri ya mtungi aijuaye kata
komaa… kaza.. kisha utapata
Siri ya mchezo naijua  mimi
tu.. na hakuna mwingine
Siri ya mchezo naijua  mimi
tu.. na hakuna mwingine

(Verse 2):Fid Q
Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma
wakati SIASA kila mara ukiwa unang’ara ujue kuna
kinara anayeunda msafara wa wanaojituma na
kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna
KIDUMU CHAMA CHA MASELA…
Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera
tuone kufuru za wenye hela
TANZANIA ni ‘  demu wa mtungo ‘ wanamuiita CHA WOOTE’’
HANGOVER .. ‘’anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote
Mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake
‘’na  gari bovu..’’  halisukumwi kwa kukaa ndani yake
MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza 
je  Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza
hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion
na daily tunafeli sababu ya  POLITICAL institutions
CIVILIZATION  imeadvance sasa wanatuua economically
hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free
Kuusaka ukweli  ni  sawa na kumenya kitunguu
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu
Ukishafika kwenye kiini  niambie nini utagundua
zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA
sasa wanaujaribu Umungu mtu kuamua leo nani atatoka

CHORUS:  ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata
komaa… kaza.. kisha utapata
Siri ya mtungi aijuaye kata
komaa… kaza.. kisha utapata
Siri ya mchezo naijua  mimi
tu.. na hakuna mwingine
Siri ya mchezo naijua  mimi
tu.. na hakuna mwingine

No comments:

Post a Comment