bongo hiphop by Fid Q ft Majani

VERSE 1:
Ulianza wewe.. wakaja waimbaji na wabana pua
Wale mwewe.. Franga wawindaji wakatusua
Kwakuwa.. wanajua mshikaji unaishi kwa miko
na zako itikadi.. ziko kimziki na sio mshiko
Kama haileti hela..basi haimake sense.. no sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi
Sikusound garbage au kuchange suddenly..
Mie ni mjeshi so naweza fight savagely
Hiphop ya ukweli.. ukapigwa radioni/sometimes malaika wa heri nao hutembelea motoni
Penzi ni kipofu na anayemuona halioni
sikuwa na hofu.. mama alinipenda tangu nikiwa tumboni
I started young.. I made my mother's womb a drum
My umblirical chord a guitar.. muhoji aliyenizaa
BONGOFLAVA mzuri kiasi.. hiphop we ndo my queen
my 1st.. my last & everything in betweenjj
 
Chorus:
Mimi na wewe.. tangu long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2
 

VERSE 2:
Kama kukupenda wewe ni dhambi.. basi shetani yu nami
na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani
For a million little pieces naweza kumcon Oprah ka James Frey
Na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee
Waufuate mkumbo huu wa wasomi.. wa midundo na mistari
ukiwa na nyundo mkononi.. ni rahisi kupigilia msumari
Sio tu bongo.. mpaka Ng'ambo hakuna uhuru wa habari
 kuna uhuru wa mwenye chombo.. mitambo na mwenye mali
Kujifanya hawasikii.. haiwasaidii.. wala haiwajengi
unachosema ni.. kamwe IPP haitompinga Mengi
Unawakumbusha wazazi wa uswazi.. chati ya uteja imeingia
na Mapusha wanauza drugs ili walishe familia
Mbaya.. kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati
mbaya zaidi ni kuwa na ndugu.. halafu kichwa maji
Amka bongo lala.. hiphop sio ufala.. ni lazima uifate
Uaminifu ni kama mshahara.. fanya kazi ili uupate

Chorus:
Mimi na wewe.. tangu long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2

VERSE 3:
Mapenzi ya sikuhizi.. bila kugombana yanakua hayana stimu
Pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu
Inanipa wazimu.. kusikia kimwana haujaachana na Hasheem
Na bado mnawasiliana..una mpango wa kuchanganya timu?
Nakupenda hiphop.. ndo maana ninarap ile mbaya
Naspit fire bila hennessy.. au kula kaya
I want my art to be my legacy.. kabla sijaretire.. waanze nigwaya hawa enemies.. anyways NI HAYO TU
Beef huletwa na wivu.. na wivu sio hiphop

No comments:

Post a Comment