mademu lyrics by mpoki ft barnaba


It’s talk of the time classic
Fish crab music lamar
Fish crab representing mpoki barnaba
Fish crab cook out
aaaah
(verse1)
Mwanamke lazima awe na sifa kubwa tatu
Kwanza awe anajiheshimu mtaani
Mbili hodari jikoni
Na tatu mtundu chumbani
Kwa hapa Dar wanawake wamegawanyika katika sehemu kubwa mbili
Wapo wanawake wa  uswahilini na wapo wanawake wa kishua
Hapa ndio patamu
mademu wa temeke hawa wameweka sana usela mbele
maana hata uwanja wa taifa uwa wanaruka ukuta
mademu wa ilala hawa wanapenda sana chips
sijui sababu kwao kila mitaa kwao wanauza chips
ndo maana wengi ni waarabu japo hawana ndugu uarabuni
mademu wa kigogo hawa wengi wanavigimbi
kwasababu ya kupandisha   vilima kwenda visimani kuchota maji
dada zangu wa manzese ukimtongoza tu
atataka muende mkapge picha darajani

(Chorus)
Hiki Tunachokisema si kwa wote kabisa
Kama asilimia mia wao wamefika tisa
Aah ebu acheni kabisa
Aah ebu acheni kabisa


(verse2)
naingia sinza sasa eti wenyewe mnapaita kwa wajanja
mbona hata sijaona ujanja wenu
kwanza mademu wa sinza kwao kuoga mara moja kutokana na shida ya maji
mademu wa kijitonyama nao hivyo hivyo wanapenda starehe kuliko kazi na kuvaa vizuri
ukiwatongoza tu ooh nipangie nyumba upande mzima wakati hawana hata godoro
sasa ndio utajua wimbi la nyuma haliangushi chombo
mademu kwa mtogole kwa bonge gereji somanga na bila kusahau kwa bibi paka
wao hawana hata makuu wanakusubiri kwenye kitchen party hili uwapelekee vyombo
bila kusahau madada zangu wa mwembe chai wanaopenda wenzao wazae hili wawapelekee beseni
wamesahau mzao wenyewe wa binti kondo mbuzi kalamba reli

(Chorus)
Hiki Tunachokisema si kwa wote kabisa
Kama asilimia mia wao wamefika tisa
Aah ebu acheni kabisa
Aah ebu acheni kabisa


(verse3)
sasa tunaingia kwa mademu wa kishua hawa kama huna usafiri ndugu yangu uwezi kuwapata
maana wamezidi kujishembedua muda wote wanahadithiana kuhusu muvi
na kila mtu anajifanya mambo safi kuliko mwenzie
na hata kama hawana deal lazima uwaona mjini
ukiwauliza ooh unasomea nini  me nasomea airticketing mbona hamsomei busticket
ndugu yangu kama uliuza nyumba ya uridhi jiandae kujichimbia kaburi
na hata ukituma vocha ya elfu kumi hawawezi kukujibu
ukimpigia ooh me natizama prison break ngoja na me nkatizame prison clutch
kumbuka huwezi kuhairisha hitma kwa kukosa ndimu
na pesa haitolewi photocopy
nawashangaa sana tena sana hawa amdemu wa kishua
asubui wengi ni weusi na usiku wenakuwa na rangi nyeupe
huwezi amini wanavaa bukta zenye mahips kama magolikipa hili waonekane wanamahips
kidogo ooh coz yes no yes no
huwezi kwenda kwa jirani bila kutokea kwako
na mambo yakienda kombo yaache usiende nayo
mapenzi yana nguvu kuliko breakdown
watanzania kama kocha wa uiengerza alikua anaitwa Fabio kapelobasi
 sisi timu ya taifa tumtafute kocha anaitwa Fabio kibarakashia

(Chorus)
Hiki Tunachokisema si kwa wote kabisa
Kama asilimia mia wao wamefika tisa
Aah ebu acheni kabisa
Aah ebu acheni kabisa(outro)
eeh watanzania kumbukeni kabisa bado tupo pamoja
hapa unampata mpoki na barnaba kama kawaida bado tupo kwa lamar
ningependa kuwakumbusha kitu kunguru naye ni ndege ila hapandishi abiria

No comments:

Post a Comment