TAZAMA RAMANI


 ...............................................................
       

1. Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2...

2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

.......kutoka kwa admin nawatakia AMANI NA UPENDO VITAWALE KATI YETU WATANZANIA

31 comments:

  1. audio yake iko wapi mkuu

    ReplyDelete
  2. Nani mtunzi wa wimbo huu

    ReplyDelete
  3. Shukrani ni msaada mkubwa mno

    ReplyDelete
  4. KUNA BETI ANATAJWA KARUME MBONA SIJAONA?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na Mimi pia nilikuwa nashangaa

      Delete
  5. Beti ziko pungufu mbona

    ReplyDelete
  6. Quite a patriotic song quite an inspiring song

    ReplyDelete
  7. Mbona beti zipo pungufu?

    ReplyDelete
  8. Allah akuzidixhie kiongozi dah nilikuwa najua beti moja hongera kwako

    ReplyDelete
  9. Allah akuzidixhie kiongozi dah nilikuwa najua beti moja hongera kwako

    ReplyDelete
  10. Huu wimbo hauna nota zake mwenye pdf yake naiomba tafadhali

    ReplyDelete
  11. Nakupenda sana Tanzania

    ReplyDelete
  12. Asanteni mungu awabariki

    ReplyDelete
  13. Nimeipenda weka audio

    ReplyDelete
  14. Wimbo mzuri wa uzalendo; mwenye nota zake naomba

    ReplyDelete
  15. Ninafuraha sana kuona wimbo wa kizarendo ambao yeyote akiimba upendo dhidi ya nchi yake huongezeka....
    Ni mzuri mashuleni kwani unasaidia japo kwa uchache kupata viongozi makini na wazarendo

    ReplyDelete
  16. Good memory to our coming generation

    ReplyDelete
  17. Wimbo mzuri Sana huuu jamani

    ReplyDelete
  18. Kawimbo kalikoijenga haswa tanzania na utanzania

    ReplyDelete
  19. Hongera kwa mtunzi,wimbo unatupa nguvu

    ReplyDelete
  20. Asante lakini ningependa audio Mungu akubariki sana

    ReplyDelete
  21. napataje npta zake jamani tafadhali

    ReplyDelete
  22. Asante sana, lakini kuna baadhi watu wanaimba na kumtaja Hayati Karume na pia TANU.

    ReplyDelete