tamaa mbaya lyrics by 20%


sifa ya moyo tamaa, Moyo sifa yake kutamani
Tamaa ya moyo, Inaweza kukuweka matatani
Unatamani kuzaa, wakati bado upo shuleni
tumia akili kukataza, kabla hujawa matatizoni
ile ndoto ya kitandani, achana nayo!
kama unahisi labda, haiwezekani kuendana nayo!
unaweza kuota umejenga angani, angani
kuiihifadhi ndoto ya shida gani, wewe!

tuliza moyo wako
kubali mapungufu yako
rahisisha mahitaji yako
ongeza kipato chako
Chunga, tamaa mbaya
Chunga, tamaa mbaya
Chunga, tamaa mbaya
Chunga, tamaa mbaya x 2

sifa ya macho kuona, yaani kutazama kinachoonekana
ila sio kila unachokiona ukazana kupata inawezekana
nyumbani kuna msichana, njiani utaona wengi wasichana
bora kuishia kutazama, kuliko kujifanya unaweza sana
siri ya maisha yako ipo kwa muumba, muumba
alisema mbuzi ni mbuzi hawezi kuwa simba, kuwa simba!
hawezi kuongea eti anafosi kuimba,
bora kutulia ama kupiga marimba utasikika pia

tuliza moyo wako
kubali mapungufu yako
rahisisha mahitaji yako
ongeza kipato chako
Chunga, tamaa mbaya
Chunga, tamaa mbaya
Chunga, tamaa mbaya
Chunga, tamaa mbaya x 2

mwanzo wa safari nakufuata kijana, nakuja na swali nipe jibu la maana
dunia bila wizi hivi itawezekana, kama haiwezekani siku tukishaonana..
wanipige kabali ki simu changu cha Mchina
vijana wote nitawaona hamna maana, sana
tunarudishana nyuma mambo ya kuibiana
Mwenzenu naona noma polisi kupelekana, yeah

tuliza moyo wako
(eeh, tuliza moyo tuliza moyo mzee)
kubali mapungufu yako (eh kubali kuwa vitu fulani, huna!)
rahisisha mahitaji yako (eh sio lazima uwe na vikubwa!)
ongeza kipato chako (eh ongeza kipato utapata unachotaka)
Chunga, tamaa mbaya (tamaa mbaya!)
Chunga, tamaa mbaya
Chunga, tamaa mbaya
Chunga, tamaa mbaya
tuliza moyo wako (tulizaaaa, tulizaaaa!)
kubali mapungufu yako (kubali kubali)

2 comments:

  1. Nampenda sana 20paa,naitwa TOPN B,nipo kalemie.
    maisha ya bongo,huyu jamaa noma sana...Reds...Kwetu nyumbani drc anapendwa sana 20paa.

    ReplyDelete
  2. Wow I just love the song, a song that won't die,,, but (sponsors and these ladies waaah)

    ReplyDelete